Pangilia Herufi na Akili 1.0.0 Icon

Pangilia Herufi na Akili

Ubongo Educational
4.5
34 Ratings
10K+
Downloads
1.0.0
version
Oct 12, 2019
release date
66.0 MB
file size
Free
Download

About Pangilia Herufi na Akili Android Game

Labda mtoto wako ameanza kujifunza alfabeti au ameanza kujifunza kupanga maneno, Pangilia herufi na Akili itamsaidia kuwa mpanga herufi mzuri mwenye kujiamini!

KWANINI UPAKUE PANGILIA HERUFI NA AKILI?

- NGAZI: Kila ngazi inayofuata ina changamoto zaidi kuliko iliyopita
- UBORA: imetengenezwa na timu ya watu waliobobea katika fani za elimu/ ufundishaji, uhandisi wa programu za simu ya mkononi, wabunifu wa michoro/ picha, watengenezaji wa katuni na uhandisi wa sauti
- UHAKIKISHO: Programu hii imebuniwa kulingana na matokeo ya utafiti ya jinsi watoto wadogo wanavyoweza kujifunza vizuri zaidi
- UTAMBULISHO: Akili ni mtoto mwenye miaka minne, mdadisi, mwerevu na anayependa kujifunza… mfano wa kuigwa kwa watoto wote

JINSI INAVYOFANYA KAZI

Chagua kati ya ngazi 16 kuanzia rahisi hadi ngumu! Kila ngazi inamkusanyiko wa maneno saba ya kupangilia, huku Ikiwa imepangiliwa kama mchezo na kuambatana na picha. Neno litatamkwa kwa sauti.

Kwenye ngazi rahisi, mpira wenye herufi utaondolewa kwenye neno na mchezaji atatakiwa kujaza herufi kwenye neno kwa kuweka mpira wenye herufi mahali sahihi. Kwenye ngazi ya juu, mipira tofauti tofauti yenye herufi imeondolewa hivyo mchezaji!

Kupangilia herufi, shika na usogeze mipira yenye herufi. Utakapokuwa unaisogeza utasikia matamshi ya herufi. Ukifanikiwa kuiweka mahali sahihi itabaki hapo, kama sivyo itarudi pale ulipoitoa.

FAIDA ZA KUJIFUNZA

* Jifunze na kuzoea kupangilia maneno kwa usahihi
* Jifunze uwezo wa kushirikisha mikono na macho
* Jifunze kutokata tamaa, jaribu mpaka ufanikiwe
* Cheza mwenyewe
* Furahia kucheza huku unajifunza


VIPENGELE MUHIMU

- Maneno 136 yaliyoambatana na picha
- Matamshi sahihi ya herufi na maneno
- Programu hii ni mahali salama kwa ajili ya mtoto wako kucheza
- Kwa ajili ya watoto wenye miaka mitatu, minne, mitano na sita
- HAKUNA maksi za juu, hivyo hakuna kushindwa wa la mkazo
- Inafanya kazi bila intaneti

JARIBU APP KATIKA KIINGEREZA

Kujifunza maneno yaliyo muhimu katika kiingereza, pamoja na jinsi ya kupangilia herufi zake, pakua App ya Spelling with Akili https://play.google.com/store/apps/details?id=com.enuma.ubongo.SpellingEN

KIPINDI CHA TELEVISION - AKILI AND ME

Akili and Me ni katuni zenye kuburudisha na kuelimisha kutoka Ubongo, watengenezaji wa Ubongo Kids na Akili and Me - vipindi vizuri vya kujifunza vilivyotengezwa Afrika kwa ajili ya Waafrika.

Akili ni mtoto mwenye miaka minne na mwenye udadisi, anaishi na famiia yake karibu na mlima Kilimanjaro, nchini Tanzania. Ana siri moja,kila usiku anapokuwa amelala, anaingia kwenye ulimwengu wa maajabu unaoitwa Lala land, ambako yeye na marafiki zake ambawo ni wanyama tofauti tofauti wanajifunza lugha, herufi, nambari na sanaa na wakati huohuo akijifunza ukarimu na kuanza kupatwa na hisia na mabadiliko ya haraka ya maisha ya mtoto mdogo!

Angalia video za Akili and Me kwenye mtandao au tembelea kwenye tovuti ya www.ubongo.org ili ujue kama vipindi vinaonyeshwa katika nchi yako.

KUHUSU UBONGO

Ubongo ni shirika la kijamii linalotengeneza vipindi vyenye kuelimisha na kuburudisha kwa ajili ya watoto barani afrika kwa kutumia teknolojia ambazo wanazo. Tunawaburudisha watoto waweze KUJIFUNZA na KUPENDA KUJIFUNZA!

Tunatumia nguvu ya burudani, vyombo vya habari, na simu za mkononi kuwafikishia vipindi vyenye ubora wa hali ya juu, kuelimisha, kuburudisha na vilivyotengenezwa kwa ajili ya mazingira yetu.

KUHUSU CURIOUS LEARNING

Curious learning ni shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na kusambaza maudhui ya kujifunza kwa kila anaehitaji. Sisi ni timu ya watafiti, wasanidi programu na waelimishaji tuliojikita katika kuwapa watoto waliopo mahali popote na elimu ya kujua kusoma na kuandika katika lugha zao za asili kwa kutumia ushahidi na data.

KUHUSU PROGRAMU

Soma na Akili - Maeneo Mengi Tofauti! Imetengenezwa na mfumo wa Curious Reader uliotengenezwa na Curious Learning kwa ajili ya kutengeneza njia ya kusoma yenye kumhusisha mtumiaji.

Other Information:

Requires Android:
Android 4.4+ (Kitkat, API 19)
Other Sources:

Download

This version of Pangilia Herufi na Akili Android Game comes with one universal variant which will work on all the Android devices.

Variant
1
(Oct 12, 2019)
Architecture
arm64-v8a armeabi-v7a
Minimum OS
Android 4.4+ (Kitkat, API 19)
Screen DPI
nodpi (all screens)

All Versions

If you are looking to download other versions of Pangilia Herufi na Akili Android Game, We have 1 version in our database. Please select one of them below to download.

Loading..